[19] Inafaa kwake kuswali Rak´ah mbili kujengea ya kwamba zimethibiti katika matendo ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)[1]. Bali amewaamrisha nazo Ummah wake na kusema:

“Hakika safari hii ina juhudi na uzito. Baada ya mmoja wenu kuswali Witr, basi na aswali Rak´ah mbili. Ima akaamka au akalipwa kwazo.”[2]

[20] Sunnah ni kusoma ndani yake “az-Zalzalah” na “al-Kaafiruun”.[3]

[1] Ameipokea Muslim na wengieo. Tazama “al-Irwaa´”, uk. 108-109.

[2] Ameipokea Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” yake. Imetajwa katika “as-Swahiyhah”. Nilikuwa nimechukua msimamo wa kunyamaza juu ya Rak´ah mbili hizi kwa muda mrefu. Nilipoona amri hii ya kiutume tukufu, nikakimbilia kuitendea kazi na nikatambua maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Ifanyeni swalah yenu ya mwisho iwe ni Witr” ni kwa minajili ya khiyari, na sio malazimisho. Haya ndio maoni ya Ibn Naswr (130).

[3] Ameipokea Ibn Khuzaymah (1104) na (1105) kutoka katika Hadiyth ya ´Aaishah na Anas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kwa sanadi mzili zinazopeana nguvu. Tazama “Swifat-us-Swalaah”, uk. 124.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qiyaam Ramadhwaan, uk. 33
  • Imechapishwa: 07/05/2019