13. Qur-aan kwa mujibu wa Ahl-us-Sunnah

Ahl-us-Sunnah wanaonelea kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah aliyozungumza. Kuna dalili tele zinazofahamisha kuwa Allaah anazungumza na kuita. Siku ya Qiyaamah Allaah atawaita waumini na makafiri:

وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ أَيْنَ شُرَكَائِي قَالُوا آذَنَّاكَ مَا مِنَّا مِن شَهِيدٍ

“Siku Atakayowaita: “Wako wapi [sasa] washirika Wangu?” Watasema: “Tunakiri Kwako hapana miongoni mwetu awezaye kushuhudia [hayo kuwa wapo].” 41:47

وَإِذْ نَادَىٰ رَبُّكَ مُوسَىٰ أَنِ ائْتِ الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ

“[Unakumbuka] pindi Mola wako Alipomwita Muusa [na kumwambia]: “Nenda kwa watu madhalimu.” 26:10

Katika Aayah nyingi Allaah ametukhabarisha kuwa alikuwa na mazungumzo ya manongonezo nae na vilevile akamwita. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

وَاللَّـهُ يَقُولُ الْحَقَّ وَهُوَ يَهْدِي السَّبِيلَ

“Allaah anasema ya haki Naye ndiye aongozaye njia [iliyonyooka].” 33:04

Qur-aan inaeleza wazi kwamba Allaah anasema na kuzungumza na kwamba amezungumza kwa Qur-aah hii iliyoteremka kutoka Kwake:

تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ

“[Hapana,] ni uteremsho kutoka kwa Mwenye hikmah wa yote, Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote.” 41:42

Maneno haya asli yake ni yenye kutoka kwa Allaah (Tabaarak wa Ta´ala). Amemfunulia nayo Jibriyl na Jibriyl akamfikishia nayo Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ahl-ul-Ahwaa´ wana upotevu na kujigonga kunakopingana na Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amewawafikisha Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah haki na usawa katika mambo yote haya ambayo kuna maoni tofauti juu yake. Kwa kuwa wameshikamana na Kitabu cha Mola wao na Sunnah za Mtume wao (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanaitakidi kuwa maneno ya Allaah ni haki na kwamba Allaah hasemi isipokuwa haki tu. Kusemwe nini sasa juu ya yule ambaye haonelei kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah na anaonelea kuwa imeumbwa?

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qurrat-ul-´Aynayn bi Tawdhwiyh Ma´aaniy ´Aqiydat-ir-Raaziyayn, uk. 23-24
  • Imechapishwa: 15/10/2016