13. Ni wajibu kwa mwanamke kufunika miguu yake anapotoka nyumbani

4- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah hatomwangalia mtu mwenye kuburuta mavazi yake kwa kiburi.” Umm Salamah akasema: “Wanawake wafanye nini na viburuta vyao?” Akasema: “Wafanye iwe shibri moja.” Akasema: “Miguu yao itaonekana.” Ndipo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Wafanye iwe dhiraa moja na wasizidishe.”[1]

Hadiyth hii inatolea dalili kuonyesha kuwa ni wajibu kwa mwanamke kufunika miguu yake, jambo ambalo lilikuwa linajulikana kwa wanawake wa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Ni jambo lisilokuwa na shaka kuwa miguu ni yenye fitina kidogo kuliko uso na vitanga vya mikono. Uzinduzi juu ya kidogo kwa dhati yake ni uzinduzi juu ya kikubwa. Shari´ah yenye hekima haiwezi kuwajibisha kitu kilicho na fitina kidogo kufunikwa na kuruhusu kilicho na fitina kidogo kuonyeshwa. Ni mgongano usiyowezekana kwa hekima na Shari´ah ya Allaah.

[1] at-Tirmidhiy (1731) na an-Nasaa´iy (5338).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hijaab, uk. 18-19
  • Imechapishwa: 26/03/2017