13. Ni ipi hukumu ya kutumia sindano za kawaida zinazodungwa kwenye mishipa na kwenye misuli?

Swali 13: Ni ipi hukumu ya kutumia sindano za kawaida zinazodungwa kwenye mishipa na kwenye misuli? Ni ipi tofauti baina yazo kwa mfungaji?

Jibu: Maoni ya sawa ni kwamba hazifunguzi. Hakuna sindano zinazofunguza isipokuwa tu zile za lishe. Kadhalika kuchota damu kwa sababu ya kipimo hakumfunguzi mwenye kufunga. Kwa sababu kitendo hichi sio kama kufanya chuku. Kuhusu kupiga chuku kunamfunguza yule mwenye kufanya na mwenye kufanyiwa kwa mujibu wa maoni yenye nguvu ya wanachuoni. Hayo ni kutokana na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Amefungua mwenye kufanya chuku na mwenye kufanyiwa.”[1]

[1][1] Abu Daawuud (2367) na Ibn Maajah (1680).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdllaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah Muhimmah tata´alaqah bisw-Swiyaam, uk. 21-22
  • Imechapishwa: 22/04/2019