Miongoni mwa yale atakayopewa huko Aakhirah ni kile Cheo chenye kusifiwa ambacho hakuna yeyote ambaye atakisogelea. Abu Bakr Ahmad bin Abiy Khaythamah amesimulia kwa cheni ya wapokezi wake kutoka kwa Mujaahid ambaye amesema kuhusu maneno Yake:

عَسَىٰ أَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامًا مَّحْمُودًا

“Hakika Mola wako akakuinua cheo kinachosifika.”[1]

”Atamkaza juu ya ´Arshi.”[2]

Abu Bakr bin Abiy Shaybah na ´Uthmaan bin Abiy Shaybah wamepokea kwa cheni za wapokezi wao kutoka kwa Mujaahid ambaye amesema kuhusiana na Aayah hiyohiyo:

”Atamkaza juu ya ´Arshi.”

Kadhalika ´Abdullaah bin Ahmad amepokea kwa cheni ya wapokezi wake kutoka kwa Mujaahid. Vivyo hivyo amepokea Ishaaq bin Raahuuyah kutoka kwa Ibn Fudhwayl kutoka kwa Layth kutoka kwa Mujaahid ambaye amesema kuhusiana na Aayah hiyohiyo:

”Atakaa pamoja naye juu ya ´Arshi.”

Ibn ´Umayr amesema:

”Nimemsikia Abu ´Abdillaah Ahmad bin Hanbal akiulizwa kuhusu Hadiyth ya Mujaahid ambapo akasema: ”Wanachuoni wameinukuu kwa kuikubali na hivyo tunaipitisha kama ilivyokuja.”

Ibn-ul-Haarith amesema:

”Ndio, Muhammad atakazwa juu ya ´Arshi.”

´Abdullaah bin Ahmad amesema:

”Mimi namkemea kila yule ambaye anairudisha Hadiyth hii.”

Ibn ´Abbaas amesema kuhusiana na Aayah hiyohiyo:

”Atamkaza juu ya ´Arshi.”

Mapokezi haya yamepokelewa na Shaykh wetu Abu Bakr al-Marwaziy na akatunga kitabu kikubwa juu ya maudhui hayo. Kadhalika ameeleza baba yangu kutoka kwake kwa cheni ya wapokezi wake kutoka kwa Ibn ´Umar kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusiana na Aayah hiyohiyo:

”Atakaa pamoja naye juu ya kiti.”

Kadhalika kwa cheni ya wapokezi kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye amesema:

”Nilimuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu Cheo chenye kusifiwa. Akasema: ”Mola wangu ameniahidi kukaa juu ya ´Arshi.”

Vivyo hivyo kwa cheni ya wapokezi kutoka kwa Ibn ´Umar ambaye amesema:

”´Umar bin al-Khattwaab alisema kunambia: ”Nilimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kile alichomuahidi Mola wake Akasema: ”Ameniahidi Cheo chenye kusifiwa ambacho ni kukaa juu ya ´Arshi.”

Vilevile ana Hodhi hiyo siku ya Qiyaamah.

[1] 17:79

[2]Taariykh Ibn Abiy Khaythamah.

  • Mhusika: Imaam Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-I´tiqaad, uk. 37-40
  • Imechapishwa: 26/02/2019