13. Mlipuko wa Khubar ni mfano wa ugaidi


12- Ulipuaji wa mwisho uliotokea siku ya jumanne tarehe 09 Swafar mwaka wa 1417 Khubar mashariki mwa Saudi Arabia ni mfano mwingine wa kutisha wa ugaidi uliofanywa na watu madhalimu.

Kwa sababu ya matokeo yake mlipuko huu wa mwisho ulikuwa mbaya zaidi kuliko ule wa ar-Riyaadh. Waislamu na makafiri wengi waliopewa amani walikufa na kujeruhiwa. Watu wengi wenye amani nchini waliingiwa na khofu na woga. Vivyo hivyo wale wenye kutembelea nchi kupitia serikali. Hilo lilipelekea vilevile kupata khasara kubwa katika miradi iliyokamilika miezi michache iliyopita. Tunamuomba Allaah asahilishe wale wahalifu magaidi watiwe mbaroni ili waweze kuhukumiwa na Shari´ah ya Allaah na iwe ni ukumbusho kwa wale wasioogopa jengine isipokuwa tu upanga wa haki unaotekelezwa na kiongozi.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Irhaab, uk. 20
  • Imechapishwa: 14/04/2017