13. Mke mwema hapeani mali bila idhini ya mume

7 – Hatoi kutoka katika mali yake mume wala mali ya mke wake isipokuwa kwa idhini yake mume. ´Abdullaah bin ´Amr al-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Haijuzu kwa mwanamke kutoa zawadi isipokuwa kwa idhini ya mume wake.”[1]

al-Albaaniy amesema:

“Lakini haitakikani kwa muislamu – kama kweli ni muislamu wa kweli – kutumia vibaya hukumu hii ambapo akamfanyia dhuluma mke wake ambapo akamzuilia katika mali yake katika mambo yasiyokuwa na madhara kwao wote wawili. Haki hii imefanana na haki ya walii wa msichana ambaye haijuzu kwake msichana kujioza mwenyewe pasi na idhini ya walii wake. Ikiwa atamzuilia, basi atapeleka mashtaka kwa Qaadhiy anayekubalika katika Shari´ah ili amfanyie uadilifu. Basi vivyo hivyo hukumu ya mali ya mwanamke wakati mume wake atapomfanyia dhuluma ambapo akamzuilia kuitumia mali yake katika mambo yanayokubalika kwa mujibu wa Shari´ah. Katika hali hiyo Qaadhiy vilevile atamfanyia uadilifu. Hapana ishkali kutumika hukumu hiyohiyo. Matatizo yanakuja pale ambapo mke ataitumia vibaya. Kwa hivyo zingatia jambo hilo!”[2]

[1] Ameipokea kwa tamko hili Abu Daawuud (3547), an-Nasaa´iy (05/65-66) na Ahmad (02/179 na 184). Ni nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “as-Swahiyhah” (02/493).

[2] Silsilah Ahaadiyth-is-Swahiyhah (02/420).

  • Mhusika: Shaykh Muhammad Shuwmaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 29-31
  • Imechapishwa: 27/09/2022