13. Mfano wa nne wa hekima ya Mtume (صلى الله عليه وسلم)

Ni kuhusu kisa cha ambaye alikuwa amevaa pete ya dhahabu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa amebainisha kuwa dhahabu ni haramu kwa wavulana wa Ummah huu. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hivi kweli anakusudia mmoja wenu kuweka kaa kutoka Motoni na akaliweka mkononi mwake?”

Halafu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamvua nayo na kuitupa. Aliposhika njia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwenda zake yule mtu akaambiwa: “Chukua pete yako na unufaike nayo.” Akasema: “Ninaapa kwa Allaah! Sichukui pete iliyotupwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Katika matangamano haya kuna aina fulani ya mtu huyu kufanyiwa ususuwavu. Udhahiri ni kuwa mtu huyu alikuwa amefikiwa na khabari ya kwamba dhahabu ni haramu kwa wanaume wa Ummah huu. Kwa ajili hii ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitangamana na mtu huyu kwa ukali kidogo kuliko alivyotangamana na wale tuliowataja karibuni.

Kwa hivyo ni lazima kwa mlinganizi amteremshe kila mmoja katika ngazi yake kwa kiasi na vile inavyopelekea hali yake. Kuna mjinga asiyejua. Kuna ambaye ni mjuzi lakini hata hivyo yuko na uzembe na uvivu. Mwingine ni mjuzi lakini hata hivyo ni mkaidi na ni mwenye jeuri. Hivyo basi, ni wajibu kumteremsha kila mmoja katika hawa ngazi anayostahiki.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dawr-ul-Mar´ah fiy Iswlaah-il-Mujtama´ https://www.sahab.net/home/?p=806
  • Imechapishwa: 02/02/2017