13. Mfano wa nane kuonyesha jinsi Raafidhwah wanavodai kuwa Maswahabah wamepotosha Qur-aan

al-Kulayniy amesema:

“Abu ´Aliy al-Ash´ariy amepokea kutoka kwa Muhammad bin ´Abdil-Jabbaar, kutoka kwa Swafwaan, kutoka kwa Ishaaq bin ´Ammaar, kutoka kwa Abu Baaswiyr, kutoka kwa Abu Ja´faar ambaye amesema:

“Qur-aan imeteremshwa ikiwa robo nne (1/4); moja ni kuhusu sisi, nyingine kuhusu maadui zetu, nyingine ni kuhusu watu waliotangulia na mifano na nyingine kuhusu mambo ya faradhi na hukumu.”[1]

Iko wapi sehemu ya Tawhiyd iliyojengwa katika ulinganizi wa Mitume wote? Qiyaamah na malipo viko wapi? Kiko wapi hiki na kile?

Isitoshe, ni vipi tutaoanisha baina ya mapokezi haya yenye kugongana? Mapokezi ya ´Aliy (Radhiya Allahu ´anhu) yanasema kuwa Qur-aan imeteremshwa ikiwa theluthi; moja inahusu sisi na nyingine maadui zetu na kadhalika. Mapokezi ya Ja´faar yanasema kuwa Qur-aan imeteremshwa ikiwa robo nne; moja inahusu sisi na nyingine inahusu maadui zetu na kadhalika. Ukweli wa mambo ni kwamba Allaah hakuteremsha si robo nne wala robo sita kuhusu watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na maadui zake kutokana na matusi na Takfiyr.

Makusudio ya robo nne zilizozushwa zinazohusiana na maadui wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Maswahabah na sio washirikina, mayahudi, manaswara wala waabudu moto. Waislamu hawawezi kupata neno hata moja linaloashiria kuwa Maswahabah wanawachukia watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuwapora haki zao. Kitu wanachoweza kupata tu ndani ya Qur-aan ni jinsi wanavosifiwa na kutapwa kwa hali ya juu.

Swali langu kwa hawa waongo ni: Kwa nini hamtaji Tawhiyd na maadui wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoka katika washirikina, mayahudi, manaswara na waabudu makaburi? Ni kwa sababu nyinyi ni maadui wa Tawhiyd na watu wake na washirika wa washirikina, mayahudi na wengine. Ni vipi mnaweza kuwakemea washirikina wakati nyinyi ni washirikina wakubwa zaidi yao? Na ni vipi mnaweza mkawakemea juu ya kumsemea Allaah uongo na kupotosha dini Yake na ujumbe Wake wakati hawako hata karibu na yote hayo mliyoyataja?

[1] al-Kaafiy (02/628).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 41-42
  • Imechapishwa: 19/03/2017