17. Matahadharisho ya kukaa na Ahl-ul-Ahwaa´

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanatahadharisha vikali kabisa kukaa na Ahl-ul-Ahwaa´ wal-Bid´ah, kwa sababu kukaa nao ni kwenda kinyume na maamrisho ya Allaah. Isitoshe ni alama ya kuwapenda. Vilevile kunachelea kwa yule mwenye kukaa nao akajisalimisha na upotevu wao na akawafuata katika batili yao. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Bid´ah ambayo mtu anazingatiwa kwayo ni katika Ahl-ul-Ahwaa´ ni zile zenye kujulikana kwa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah zinazoenda kinyume na Qur-aan na Sunnah. Mfano wa Bid´ah hizo ni kama Bid´ah ya Khawaarij, Raafidhwah, Qadariyyah na Murjia-ah.”

Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِذَا رَأَيْتَ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ الشَّيْطَانُ فَلَا تَقْعُدْ بَعْدَ الذِّكْرَىٰ مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ

“Na unapowaona wale wanaoziingilia Aayah Zetu, basi jitenge nao mpaka waingie katika mazungumzo mengineyo. Na kama shaytwaan atakusahaulisha, basi baada ya kukumbuka, usikae pamoja na watu madhalimu.” (06:68)

Ibn ´Abbaas amesema:

“Kila mwenye kuzua katika dini ameingia katika Aayah hii na kila mzushi mpaka siku ya Qiyaamah.”

Haya yamenukuliwa kutoka kwa al-Baghawiy katika Tafsiyr yake. Ibn Jariyr at-Twabariy amesema:

“Katika Aayah hii kuna dalili ya wazi kabisa juu ya makatazo ya kukaa na watu wa batili kwa sampuli zote za wazushi na watenda madhambi pindi wanapoingia ndani ya batili yao.”

Ibn ´Abbaas amesema:

“Usiikae na Ahl-ul-Ahwaa´, kwa kuwa kukaa nao kunazigonjwesha nyoyo.”

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mu´taqad as-Swahiyh, uk. 99-100
  • Imechapishwa: 22/06/2020