13. Masharti ya ndoa ni lazima yatimizwe

Miongoni mwa haki za wanandoa wakati wa kufunga ndoa ni pamoja na kwamba yule ambaye atakubali kwa khiyari yake masharti [fulani] ni wajibu juu yake kuyatimiza. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Masharti ambayo ni wajibu zaidi kwenu kuyatimiza ni yale mliyofanyiwa halali kwa tupu zenu.”[1]

Imethibiti kuwa mwanaume mmoja aliemuoa mwanamke ambaye alikubaliana naye kutomtoa kwenye nyumba yake. Sharti ya mwanamke ilikuwa asimtoe nyumbani kwake na akakubali sharti hiyo. Baada ya kumuoa akataka kumtoa. Wakapeleka magomvi kwa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye alisema:

“Ana haki ya sharti yake.”

Bi maana ni wajibu kwako kutimiza sharti hiyo.

Mwanaume yule akasema: “Basi tutenganishe.” ´Umar akasema: “Haki ni zenye kukatika wakati wa masharti.”[2]

[1] al-Bukhaariy (2721) na Muslim (1418).

[2] al-Bukhaariy ameitaja bila ya mnyororo. Imepokelewa kwa mnyororo wenye kuunganishwa kwa Ibn Abiy Shaybah (16449), Sa´iyd bin Mansuur (622) na (680) na al-Bayhaqiy (7/14438).

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 19-20
  • Imechapishwa: 24/03/2017