1- Imependekezwa kuharakisha kukata swawm pale kunapohakikishwa kwa macho kuwa jua limezama au mtu akaelezwa na mtu mwaminifu na mwadilifu. Hayo ni kutokana na yale yaliyothibiti kwa al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa Sahl bin Sa´d (Radhiya Allaahu ´anh) aliyeeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wato hawatoacha kuwa katika kheri muda ya kuwa wanaharakisha kukata swawm.”

  Hayo ni kwa sababu kuharakisha kukata swawm kunafahamisha utekelezaji [wa maamrisho ya Allaah] na kuchelewesha kunafahamisha kuchupa mipaka. Hayo yanafanywa na mayahudi na manaswara na baadhi ya mapote yaliyopinda ambayo yanachelewesha kukata swawm mpaka kunachomoza nyota. Katika “as-Sunan” ya Abu Daawuud imepokelewa:

“Mayahudi na manaswara ndio wenye kuchelewesha.”

Ibn Hibbaan na al-Haakim wamepokea kupitia kwa Sahl (Radhiya Allaahu ´anh) kwa tamko linalosema:

“Ummah wangu utaendelea kuwa juu ya mwenendo wangu muda wa kuwa wakati wa kukata kwao swawm hawasubiri kuchomoza kwa nyota.”[1]

[1] Ibn Hibbaan (3510) na al-Haakim (1584) ambaye amesema:

”Hadiyth hii iko kwa mujibu wa masharti ya al-Bukhaariy na Muslim na hawakuipokea kwa mtiririko kama huu.”

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtaswaru fiy Ahkaam-is-Swiyaam, uk. 19
  • Imechapishwa: 23/05/2019