13. Madhara ya wale wanaojifanya ni wanazuoni

Imaam Ibn ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Na ubainifu wa yule mwenye kujifananisha… – Makusudio ni kubainisha mwenye kujifananisha na wanazuoni ilihali sio katika wanazuoni. Anataka kujipenyeza na kujifananisha na wanazuoni ilihali ni mtupu inapokuja katika mambo ya elimu. Huyu madhara yake ni makubwa kwake mwenyewe na kwa ummah kwa kuwa anazungumza juu ya Allaah bila ya elimu. Matokeo yake anawapoteza watu pasi na elimu. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا لِّيُضِلَّ النَّاسَ بِغَيْرِ عِلْمٍ

“Basi nani dhalimu zaidi kuliko yute anayemtungia Allaah uongo ili apoteze watu bila elimu.” (06:144)

Imesemekana:

“Watu sampuli nne wanaiharibu dunia:

1 – Mwanachuoni mbabaishaji. Huyu anaziharibu dini.

2 – Mwanasarufi mbabaishaji. Huyu anauharibu ulimi.

3 – Daktari mbabaishaji. Huyu anaiharibu viwiliwili.

4 – Mwanafalsafa mbabaishaji. Huyu anaiharibu miji.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sittah, uk. 30
  • Imechapishwa: 18/05/2021