13 – Madhambi ni mirathi ya nyumati zilizotangulia

Madhambi yote ni mirathi ya nyumati za kale ambazo Allaah aliziangamiza kwayo. Liwati ni mirathi ya watu wa Luutw. Kuchukua haki kwa ziada na kurudisha kwa kupunguza ni mirathi ya watu wa Shu´ayb. Kujinyanyua katika ardhi na kueneza ufisadi juu ya ardhi ni mirathi ya watu wa Fir´awn. Kiburi na jeuri ni mirathi ya watu wa Huud. Kwa msemo mwingine ni kwamba mtenda dhambi anajivisha moja ya vazi ya nyumati hizi na walikuwa ni maadui wa Allaah. Imaam Ahmad amepokea katika “al-Musnad” yake kupitia Hadiyth ya ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambaye amesimulia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:

“Atakayejifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”

  • Mhusika: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Daa’ wad-Dawaa’, uk. 69
  • Imechapishwa: 07/01/2018