13. Kuhirimia kwa ajili ya hajj siku ya Tarwiyah

58- Itapokuwa siku ya Tarwiyah, nayo ni ile siku ya nane katika Dhul-Hijjah, ndipo atahirimia na atahirimia kwa ajili ya hajj. Atafanya kama yale aliyoyafanya wakati wa kuhirimia ´Umrah kule katika vituo; kuoga, kujitia manukato, kuvaa Izaar na kishale na kuleta Talbiyah. Wala asiikate [hiyo Talbiyah] isipokuwa kabla ya kutupa mawe katika nguzo ya ´Aqabah.

59- Atahirimia mahali ambapo yeye ameshukia. Hata watu wa Makkah watahirimia kutokea Makkah.

60- Kisha atakwenda Minaa na kuswali hapo swalah ya Dhuhr. Vilevile atalala Minaa mpaka aswali swalah zote tano. Swalah hizi zinatakiwa kufupishwa na zisijumuishwe.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manaasik-ul-Hajj wal-´Umrah, uk. 27-28
  • Imechapishwa: 15/07/2018