13. Kisa cha Nuuh katika Taurati na Qur-aan

Mfano wa hilo ni kisa cha Nuuh (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanasema kwa kukata kabisa ya kwamba kisa hiki Qur-aan imekichukua kutoka kwenye Taurati. Hata hivyo iliteremshwa Makkah katika zama ambazo hapakuwa myahudi hata mmoja. Wajuzi wa kuandika na wa kusoma walikuwa wachache mno kabisa na hapakuwa uadui wowote kati yao na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa hawezi kuandika wala kusoma. Maadui wake walikuwa chini ya uangalizi wake. Wanapoona msomi anaenda kwake au yeye anaenda kwa msomi, wanamkaripia. Kisa cha Nuuh katika Taurati kimesimuliwa kwa upambanuzi na kumeelezwa kwa urefu na upana wake. Wakanamungu wametumia fursa ya usimulizi huu kuitukana Taurati. Wanasema kuwa meli ilio kwa sura kama hii haiwezi kutulia ndani ya bahari dakika hata moja. Hata hivyo hawawezi kusema hayo juu ya kisa hicho katika Qur-aan.

Vilevile wametumia fursa ya maelezo ya ardhi na jiografia ya Taurati ili kutukana usahihi wake. Hata hivyo hawakupata kitu katika Qur-aan cha kupitisha malengo yao. Mwenye kusoma kisa cha Nuuh katika Qur-aan na kisa hicho katika Taurati ataona tofauti kubwa kati yake. Utaona kuwa njia iliyotumiwa katika Qur-aan ni ya kiungu na ya kuvutia na ina mazingatio, matahadharisho na bishara njema. Ni jambo lililo mbali kabisa na njia ya uanadamu. Njia iliyoko katika Taurati ni kinyume kabisa.

Wasipopata athari yoyote katika Taurati, Injili au Talmud, kwa mfano kisa cha Luqmaan, wanasema kuwa kisa ni ngano na ukhurafi wa waarabu. Wakati huo huo wanaandika vichwa vya khabari kwenye Taurati na Injili kwa maji ya dhahabu “Biblia”. Hata hivyo hayawaumi maadui wa kanisa. Wanakosoa vibaya sana vitabu vya mayahudi na wakristo.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad Taqiyy-ud-Diyn al-Hilaaliy al-Maghribiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Baraahiyn al-Injiylyyah ´alaa anna ´Iysaa daakhil fiyl-´Ubuudiyyah wa la hadhdhwa lahu fiyl-Uluuhiyyah, uk. 33-34
  • Imechapishwa: 16/10/2016