14. Hitimisho


Hizi ni baadhi ya sifa za mke mwema ambazo nimezikusanya kutoka katika maandiko ya Allaah (´Azza wa Jall) na Sunnah za Mtume Mtukufu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Nimefanya hivyo kwa kutaraji kwa M ola (Subhaanah) Amnufaishe kwazo yule Amtakaye katika waja Wake. Kwani Yeye pekee ndiye Mwenye kuwafikisha.

Ninamuomba Allaah (Jalla wa ´Alaa) kwa majina Yake mazuri kabisa na sifa Zake kuu Atuongoze sote katika njia iliyonyooka, afanye yale tunayojifunza yawe ni hoja kwetu na si dhidi yetu, Atubariki katika maneno yetu, matendo yetu, wakati wetu, wake zetu, watoto wetu, mali zetu na maisha yetu yote, Atutengenezee dini yetu ambayo ndio kinga yetu, Atutengenezee maisha yetu ya duniani ambayo tunaishi na maisha yetu ya Aakhirah ambayo ndio kituo chetu cha mwisho, Afanye uhai kwetu kuongezeka iwe ni kheri ya kila kitu na mauti iwe ni raha kwetu kutokamana na kila shari, Awatengeneze wanawake wa waislamu na wasichana wao, Awaongoze katika njia iliyonyooka, warudi Kwake kwa njia nzuri na Awaepushe na fitina zote zilizodhahiri na zilizojificha na Atuongoze sote katika kila kheri Anayoipenda na Kuiridhia. Hakika Yeye (Tabaarak wa Ta´ala) ni Mwenye kuzisikia du´aa, Yeye ndiye wa kuwekewa matarajio, Anatutosheleza na  ndiye Mbora wa kuyasimamia mambo.

Wito wetu wa mwisho tunamhimidi Allaah, Mola wa walimwengu. Swalah, salaam na baraka zimwendee mja na Mtume Wake, mteuliwa, Muhammad bin ´Abdillaah. Allaah amsifu kwa wingi, amsalimishe, kizazi chake na Maswahabah wake wote[1].

[1] Asili ya kijitabu hiki ni muhadhara ambao nimeurekebisha kidogo lakini hata hivyo nikauacha usulubu wake ubaki kama muhadhara.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 44-45
  • Imechapishwa: 20/08/2018