13. Hekima ya kutawadha au kuoga kabla ya kulala kwa aliye na janaba


11- Hekima ya wudhuu´ huu

Hilo sio kwa njia ya uwajibu. Bali ni kwa njia ya mapendekezo yaliyokokotezwa kutokana na Hadiyth ya ´Umar aliyemuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kusema: “Je, mmoja wetu alale ilihali yuko na janaba?” Akamjibu: “Ndio, na atawadhe akitaka.”[1]

Inaitilia nguvu Hadiyth ya ´Aaishah aliyesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akilala ilihali yuko na janaba pasi na kugusa maji [hadi anapoamka baada ya hapo ndio anaoga].”[2]

Kuna upokezi mwingine kutoka kwake unaosema:

“Alikuwa akilala akiwa na janaba mpaka anapokuja Bilaal kuadhini kwa ajili ya swalah. Hapo anaamka na kuoga na hutazama namna maji yanavyomtiririka kutoka kichwani mwake. Halafu baada ya hapo anatoka na husikia sauti yake katika swalah ya Fajr. Halafu hubaki amefunga.” Muttwarif akasema: “Nikamuuliza ´Aamir: “Hapo ilikuwa Ramadhaan?” Akajibu: “Ndio, ni mamoja ikiwa Ramadhaan au miezi mingine.”[3]

[1] Ameipokea Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake (232) na wengineo.

[2] Ameipokea Ibn Abiy Shaybah (01/45/01) na waandishi wa “as-Sunan” isipokuwa an-Nasaa´iy ambaye ameipokea katika “al-´Asharah” (79-80), at-Twahaawiy, at-Twayaalisiy, Ahmad, al-Baghawiy katika “Hadiyth ´Aliy bin al-Ja´d” (01/85/09) na (02/114/11), Abu Nu´aym katika “al-Musnad” (02/224), al-Bayhaqiy, al-Haakim ambaye ameisahihisha. Mambo yako kama alivyosema kama nilivyobainisha hayo katika “Swahiyh Abiy Daawuud” kwa nambari. 223 na wengineo.

[3] Ameipokea Ibn Abiy Shaybah (02/173/02) kupitia upokezi wa Sha´biy kutoka kwa Masruuq. Mlolongo wa wapokezi ni Swahiyh. Hii ni dalili yenye nguvu kuliko ya kabla yake. Vilevile ameipokea Ahmad (06/101) na (254), Abu Ya´laa katika “al-Musnad” (01/224) na nimeipokea kwa njia nyingine tena.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 116-117
  • Imechapishwa: 08/03/2018