13. Hadiyth “Siku bora iliyochomozewa na jua ni ijumaa… “


695- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Siku bora iliyochomozewa na jua ni ijumaa. Ndani yake ndipo kaumbwa Aadam, ndipo aliingia Peponi na ndipo alitolewa ndani yake.”[1]

Ameipokea Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa´iy na Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” kwa matamshi:

“Halijapatapo jua kuchomoza wala kuzama katika siku ambayo ni bora kuliko siku ya ijumaa. Allaah amewaongoza watu kwayo na akawapoteza kutokamana nayo. Watu wanatufuata ndani yake. Hiyo ndio siku yetu. Mayahudi wana jumamosi na manaswara wana jumapili. Ndani yake mna wakati ambao hakuna muumini anayeswali na kumuomba Allaah kitu isipokuwa humpa.”[2]

[1] Swahiyh.

[2] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/434-436
  • Imechapishwa: 21/04/2017