13. Hadiyth “Hakuna mja yeyote ambaye atatawadha ambapo akafanya vizuri wudhuu´ wake… “

188 – Tha´labah bin ´Abbaad amesimulia kutoka kwa baba yake (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesema:

“Sijui ni mara ngapi nilimsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akinihadithia: “Hakuna mja yeyote ambaye atatawadha ambapo akafanya vizuri wudhuu´ wake ambapo akaosha uso wake mpaka maji yakatiririka chini ya kidevu chake, kisha akaosha mikono yake mpaka maji yakatiririka chini ya visugudi vyake, kisha akaosha miguu yake mpaka maji yakatiririka chini ya vifundo vya miguu halafu akasimama kuswali, isipokuwa atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Kabiyr” kwa cheni ya wapokezi laini.

[1] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/194)
  • Imechapishwa: 14/04/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy