13. Hadiyth “Atakayefunga siku moja katika njia ya Allaah, basi Allaah ataweka kati yake yeye na Moto… “


990- Abud-Dardaa´ (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayefunga siku moja katika njia ya Allaah, basi Allaah ataweka kati yake yeye na Moto kama mfano wa masafa kati ya mbingu na ardhi.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Awsatw” na “as-Swaghiyr” kwa cheni ya wapokezi nzuri.

[1] Nzuri kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (01/581)
  • Imechapishwa: 06/06/2018
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy