61- Baada ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kufungua Swalah alikuwa akinyamaza kidogo kabla ya kuanza kusoma. Abu Hurayrah akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Namtoa kafara baba na mama yangu. Nini unachosoma wakati unapokuwa kimya baina ya Takbiyr na kisomo?” Akasema: “Ninasema:

اللَّهُمَّ بَاعِدْ بَيْنِي وَبَيْنَ خَطَايَايَ كَمَا باعَدْتَ بَيْنَ الْمَشْرِقِ والْمَغْرِبِ اللَّهُمَّ نَقِّنِي مِنْ خَطَايَايَ كَمَا يُنَقَّى الثَّوْبُ الأَبْيَضُ مِن الدَّنَسِ اللَّهُمَّ اغْسِلْنِي مِنْ خَطَايَايَ بالثَّلْجِ والْمَاءِ والْبَرَدِ

“Ee Allaah! Niweke mbali mimi na madhambi yangu kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi. Ee Allaah! Nitakase na madhambi yangu kama inavyotakaswa nguo nyeupe na uchafu. Ee Allaah! Nisafishe na madhambi yangu kwa theluji, maji na kwa barafu.”

62- Jubayr bin Mutw´im ameeleza kwamba amemuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema katika Swalah:

الله أَكْبَرُ كَبِيراً والْحَمْدُ للهِ كَثِيراً وَسُبْحَانَ اللهِ بُكْرَةً وَأَصِيلاً ثَلاثاً أَعُوذُ باللهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيم منْ نَفْخِهِ وَنَفْثِهِ وَهَمْزِهِ

“Allaah ni Mkubwa kihakika. Himdi nyingi ni Zake Allaah. Ametakasika Allaah, Mola wa viumbe, kutokana na mapungufu asubuhi na jioni. Allaah ni Mkubwa kihakika. Himdi nyingi ni Zake Allaah. Ametakasika Allaah, Mola wa viumbe, kutokana na mapungufu asubuhi na jioni. Allaah ni Mkubwa kihakika. Himdi nyingi ni Zake Allaah. Ametakasika Allaah, Mola wa viumbe, kutokana na mapungufu asubuhi na jioni. Ninajikinga kwa Allaah kutokana na Shaytwaan aliyewekwa mbali na kiburi chake, kupulizia kwake na kutia kwake wasiwasi.”

63- ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha), Abu Sa´iyd al-Khudriy na wengineo wameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema wakati anapofungua Swalah:

سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ وَبِحَمْدِكَ وتَبَارَكَ اسْمُكَ وَتَعَالى جَدُّكَ وَلا إِله غَيْرُكَ

“Kutakasika ni Kwako, Ee Allaah na himdi zote ni Zako. Limetukuka jina Lako, Utukufu ni Wako, na hapana mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Wewe.”

64- Imepokelewa kutoka kwa ´Umar (Radhiya Allahu ´anhu) alikuwa akifanya Takbiyr na halafu ndio anasoma Du´aa ya kufungulia Swalah.

65- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaposimama kwa ajili ya Swalah anasema:

وَجَّهْتُ وَجْهِي للَّذِي فَطرَ السَّمَواتِ والأَرْضَ حَنيفاً وَما أَنا مِنَ الْمُشْرِكِينَ إِنَّ صَلاَتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي للهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ لاَ شَرِيكَ لَهُ وَبِذَلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا مِنَ الْمُسْلِمِينَ اللَّهُمَّ أَنْتَ الْمَلِكُ لاَ إِلهَ إِلاَّ أَنْتَ رَبِّي وَأَنَا عَبْدُكَ ظَلَمْتُ نَفْسِي واعْتَرَفْتُ بِذَنْبِي فَاغْفِرْ لِي ذُنُوبِي جَمِيعاً فإِنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلاَّ أَنْتَ واهْدِنِي لأَحْسَنَ الأَخْلاَقِ لاَ يَهْدِي لأَحْسَنِهَا إِلاَّ أَنْتَ واصْرِفْ عَنِّي سَيِّئَها لاَ يَصْرِفُ عَني سَيِّئَهَا إِلاَّ أَنْتَ لَبَّيْك وَسَعْدَيْكَ والْخَيْرُ كُلُّهُ في يَدَيْكَ وَالشَّرُّ لَيْسَ إِلَيْكَ أَنا بِكَ وإِلَيْكَ تَبَارَكْتَ وَتَعَالَيْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وأَتُوبُ إِلَيْكَ

“Nimeuelekeza uso wangu kwa yule ambaye Ameumba mbingu na ardhi, hali ya kumtakasia Yeye Dini yangu na sikuwa mimi ni katika washirikina. Hakika Swalah yangu na kichinjwa changu, uhai wangu na kufa kwangu ni kwa Allaah, Mola wa walimwengu, Yeye asiyekuwa na mshirika; kwa hilo nimeamrishwa na mimi ni katika Waislamu. Ee Allaah! Wewe ndiye Mfalme. Hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Wewe. Wewe ndiye Mola Wangu na mimi ni mja Wako. Nimeidhulumu nafsi yangu. Nimekiri madhambi yangu. Nisamehe madhambi yangu yote. Hakika hakuna mwengine asamehae madhambi isipokuwa Wewe. Niongoze katika tabia njema. Hakuna aongozae katika tabia nzuri isipokuwa Wewe. Niepushe na tabia mbaya. Hakuna mwengine mwenye kuepusha na tabia mbaya isipokuwa Wewe. Naitikia mwito Wako na kufuata maamrisho Yako. Kheri zote ziko Mikononi Mwako. Shari haitoki Kwako. Nimepatikana kwa ajili Yako na ni Wako. Umetakasika na umetukuka. Nakuomba msamaha na ninarejea Kwako.”

66- Wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa akiamka usiku kwa ajili ya kuswali anafungulia Swalah kwa kusoma:

اللَّهُمَّ رَبَّ جِبْرِيلَ وَمِيكَالَ وَإِسْرَافِيلَ فَاطِرَ السَّمَواتِ والأَرْضِ عَالِمَ الْغَيْبِ والشَّهَادَةِ أَنْتَ تَحْكُمُ بَيْنَ عِبَادك فِيما كانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ اهْدِنِي لِمَا اخْتُلِفَ فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بإِذْنِكَ إِنَّكَ تَهْدِي مَنْ تَشَاءُ إِلى صِرَاطٍ مُسْتَقِيم

“Ee Allaah! Mola wa Jibriyl, Mikaaiyl na Israafiyl! Muumba wa mbingu na ardhi! Wewe ambaye ni Mjuzi wa mambo yenye kujificha na yalio ya wazi! [Siku moja] utahukumu baina ya waja Wako katika mambo ambayo walikuwa wakitafautiana! Niongoze mimi katika haki katika yale waliotafautiana kwa idhini Yako – Hakika Wewe unamuongoza umtakae katika njia ilionyoka.”

67- Wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa anasimama katika Swalah sehemu ya mwisho ya usiku alikuwa akisoma:

اللَّهُمَّ لَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ نُورُ السَّمَاواتِ والأَرْضِ وَمَنْ فِيهِنَّ وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ قيّام السَّماواتِ والأَرْضِ وَمَنْ فِيهِنَّ وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ رب السماواتِ و الأرضِ و من فيهن أنت الحق وَعْدُكَ الْحَقُّ وَقَوْلُكَ الْحَقُّ وَلِقَاؤُكَ حَقٌّ والْجَنَّةُ حَقٌّ وَالنَّارُ حَقٌّ والنَّبِيُّونَ حَقٌّ وَمُحَمَّدٌ حَقٌّ وَالسَّاعَةُ حَقٌّ اللَّهُمَّ لَكَ أَسْلَمْتُ وَبِكَ آمَنْتُ وَعَلَيْكَ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْكَ أَنَبْتُ وَبِكَ خَاصَمْتُ وَإِلَيْكَ حَاكَمْتُ فاغْفِرْ لِي مَا قَدَّمْتُ وَمَا أَخَّرْتُ ومَا أَسْرَرْتُ وَمَا أَعْلَنْتُ أَنْتَ إِلهي لاَ إِله إِلاَّ أَنتَ

“Ee Allaah! Himdi zote ni Zako. Wewe ndiye nuru ya mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake. Himdi zote ni Zako. Wewe ndiye sababu ya kusimama kwa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake. Himdi zote ni Zako. Wewe ndiye Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake. Wewe ni Haki. Ahadi yako ni haki. Neno Lako ni haki. Kukutana na Wewe ni haki. Pepo ni haki. Moto ni haki. Mitume ni haki. Muhammad ni haki. Qiyaamah ni haki. Ee Allaah! Kwako nimejisalimisha. Wewe nimekuamini. Kwako nimetegemea. Kwako nimerejea. Kwa ajili Yako nimegombana. Nakuacha uhukumu. Nisamehe dhambi nilizozitanguliza na nilizozichelewesha, nilizozificha na nilizozionesha. Wewe ndiye Mola Wangu. Hapana mola anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Wewe.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 51-55
  • Imechapishwa: 21/03/2017