13. Dalili ya kuwa mwenye kumtii Mtume (صلى الله عليه وسلم) ataingia Peponi

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

… mwenye kumtii, ataingia Peponi…

MAELEZO

Hili ni haki na imechukuliwa kutoka katika maneno Yake (Ta´ala):

وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ وَسَارِعُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ

”Na mtiini Allaah na Mtume mpate kurehemewa. Na kimbilieni msamaha kutoka kwa Mola wenu na Pepo upana wake ni wa mbingu na ardhi, imeandaliwa kwa wenye kumcha Allaah. ” (Aal ´Imraan 03 : 132-133)

وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ يُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚوَذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ

”Na yeyote atakayemtii Allaah na Mtume Wake atamwingiza Pepo zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo milele – na huko ndiko kufuzu kukubwa.” (an-Nisaa´ 04 : 13)

مَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَيَخْشَ اللَّـهَ وَيَتَّقْهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَائِزُونَ

“Na yeyote yule atakayemtii Allaah na Mtume Wake na akamkhofu Allaah na akamcha, basi hao ndio wenye kufuzu.” (an-Nuur 24 :  52)

وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُولَـٰئِكَ رَفِيقًا

“Na atakayemtii Allaah na Mtume, basi hao watakuwa pamoja na wale ambao Allaah amewaneemesha miongoni mwa Manabii, wa kweli na mashahidi na waja wema – na uzuri ulioje hao kuwa ni rafiki!” (an-Nisaa´ 04 : 69)

وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا

“Na anayemtii Allaah na Mtume Wake, basi kwa hakika amefuzu kufuzu kukubwa.” (al-Ahzaab 33 : 71)

Aayah mfano wa hizi ni nyingi. Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ummah wangu wote utaingia Peponi isipokuwa yule atakayekataa.” Kukasemwa: “Ee Mtume wa Allaah, ni nani atayekataa?” Akasema: “Yule atayenitii ataingia Peponi, na yule atayeniasi ataingia Motoni.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy.

[1] al-Bukhaariy (7280) na Ahmad (2/361).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 32-33
  • Imechapishwa: 18/05/2020