13. Dalili ya kumi kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe


11- Abu ´Abdillaah bin Sadaqah al-Harraaniy ametukhabarisha: al-Faraawiy ametuhadithia: ´Abdul-Ghaafir al-Faarisiy ametuhadithia: Abu Ahmad al-Juluudiy ametuhadithia: Ibraahiym bin Muhammad bin Sufyaan ametuhadithia: Muslim bin al-Hajjaaj ametuhadithia: Ibn Abiy ´Umar ametuhadithia: Marwaan ametuhadithia: Yaziyd – Ibn Kaysaan – ametuhadithia, kutoka kwa Abu Haazim, kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ninaapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake ya kwamba hakuna mwanaume anayemwita mke wake kitandani mwake ambapo akamkatalia, isipokuwa Yule ambaye yuko mbinguni anamkasirikia mpaka pale atapomuwia radhi.”[1]

Ameipokea Muslim.

[1] al-Bukhaariy (5193) na Muslim (1436).

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 84
  • Imechapishwa: 19/04/2018