13. Dalili juu ya mguu wa Allaah 13

13- Muhammad bin ´Abdillaah ash-Shaafi´iy ametuhadithia: Ishaaq bin al-Hasan ametuhadithia: Abu Salamah Muusa bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Hammaad bin Salamah ametuhadithia, kutoka kwa Abu ´Ammaar, kutoka kwa Abu Hurayrah aliyesimulia ya kwamba alimsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

”Kutatupwa Motoni na useme:

هَلْ مِن مَّزِيدٍ

“Hakuna zaidi?”[1]

mara mbili mpaka (Tabaarak wa Ta´ala) auendee na aweke mguu Wake ndani yake. Ndipo ukusanyike na useme: “Tosha, tosha.”

[1] 50:30

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 47-48
  • Imechapishwa: 05/11/2017