13. al-Halabiy anamtuhumu Rabiy´ al-Madkhaliy kumtukana Ibn Baaz

al-Halabiy amesema:

“Imethibiti kwa sauti ya Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy akimtukana Shaykh Ibn Baaz. Vipi itakuwa ni uongo mkubwa? Je, uongo utakuwa kwenye sauti iliyothibitishwa au kwenye ukanushaji wenye kupingana na yaliyothibitishwa kwenye sauti?”[1]

Sauti inayonasibishwa kwangu imefanywa ghushi na Haddaadiyyah waongo. Walieneza uongo huu baada ya kufa Imaam Ibn Baaz. Niliwaomba kuniletea maneno yanayonasibishwa kwangu. Lau kama ingelikuwa ni kweli basi ningelienda kwa Shaykh Ibn Baaz, kutaka udhuru na kumuomba msamaha. Hawakuweza kufanya hivo kipindi ambacho Shaykh Baaz alikuwa bado yuhai. Baada ya kufa kwa miaka kadhaa ndio wakaanza kueneza sauti iliyofanywa ghushi. Hilo likamfurahisha al-Halabiy mwenye vifundo na mwongo, kwa sababu ndege hudema kwa wale wenye kufanana nao.

Mimi ni katika watu ambao wanamuheshimu kwa hali ya juu ´Allaamah Ibn Baaz na kueneza fadhila zake, utukufu wake na madonda yake. Hayo nimeyaweka kwenye vitabu vyangu, vikao vyangu na durusi zangu. Ninawanasihi vijana kusoma vitabu vyake na kujipamba kwa tabia yake.

Hali kadhalika ninamuadhimisha na kumtukuza Imaam Ahmad na kumzingatia kama Imaam wa Ahl-us-Sunnah. Ninawafunza vijana kumpenda, kumuheshimu na kumfuata.

Vilevile nimeandika hata kitabu kumtetea Imaam na Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, mfumo na ´Aqiydah yake dhidi ya mashambulizi ya mtenda dhambi mmoja Raafidhwiy. Namzingatia kuwa ni mmoja katika maimamu na Mujaddid wakubwa.

[1] Uk. 02

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=236
  • Imechapishwa: 08/01/2017