126. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa nne wa al-An´aam

al-´Ayyaashiy amesema wakati alipokuwa akifasiri:

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ قَالَ أُوحِيَ إِلَيَّ وَلَمْ يُوحَ إِلَيْهِ شَيْءٌ وَمَن قَالَ سَأُنزِلُ مِثْلَ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ

“Nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia Allaah uongi au akasema: “Nimefunuliwa Wahy” na hali hakufunuliwa Wahy wowote na yule aliyesema: “Nitateremsha mfano wa yale aliyoyateremsha Allaah.”[1]

“Abu Baswiyr amehadithia kwamba Abu Ja´far amesema: “Ina maana kwamba yule mwenye kudai uongozi asiyekuwa imamu (Rahimahu Allaah).”[2]

Aayah hii inapiga vita shirki na upotevu ambavyo ndivyo walivyotumwa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) kwa ajili ya kuja kuvipiga vita. Hakuna mtu aliye na dhuluma kubwa na uongo mkubwa kuliko yule mwenye kumjaalia Allaah mshirika katika ´ibaadah, uumbaji au kufanya kupatikana kwa kitu au akadai kuwa Allaah ana mwana. Kadhalika inahusiana na yule mtu mwenye kudai kuwa ni Mtume, kwamba Allaah anamteremshia, kwamba ana uwezo wa kupingana na Qur-aan au kwamba ana uwezo wa kuteremsha kitu mfano wa Qur-aan.

Aayah hii inawagusa vilevile Raafidhwah ambao wamewapa maimamu nafasi za Mitume. Bali wamezidi hapo na kudai kwamba wanayajua mambo yaliyofichikana. Mapokezi yao yote ya uongo kutoka kwao yamejengeka juu ya ´Aqiydah hii ya kikafiri.

Tazama namna ambavyo Baatwiniy huyu anavyopotosha maana hizi ambazo hata makafiri wa asili na waongo wanahisi haya kuyataja. Tazama jinsi anavyokuja na maana zisizopatikana hata katika Shari´ah ya Uislamu. Hakuna mwingine isipokuwa ni Ibn Sabaa´ myahudi ndiye kawawekea Shari´ah hiyo ambapo Raafidhwah Baatwiniyyah wakamfuata katika hilo.

[1] 06:93

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/370).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 184
  • Imechapishwa: 17/06/2018