124. Kueshi kati ya makaburi


Swali 124: Katika baadhi ya miji baadhi ya watu wanaishi kati ya makaburi. Ni ipi hukumu[1]?

Jibu: Wakatazwe na wakafunzwe. Haya ni maovu na kuyadharau makaburi. Wakiswali kwenye makaburi basi swalah zao ni batili. Kuketi katika makaburi kwa sura iliyotajwa na kuswali karibu nayo ni maovu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiswali kuyaelekea makaburi na msiketi juu yake.”[2]

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Laana ya Allaah iwe juu ya mayahudi na manaswara. Wameyafanya makaburi ya Mitume wao kuwa ni sehemu ya kuswalia.”[3]

Kuna maafikiano juu ya usahihi wake.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/356).

[2] Ahmad (16764) na Muslim (972).

[3] Ahmad (1887), al-Bukhaariy (1390) na Muslim (529).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 91
  • Imechapishwa: 15/01/2022