123. Ni ipi hukumu ya du´aa ya pamoja karibu na kaburi?


Swali 123: Ni ipi hukumu ya du´aa ya pamoja karibu na kaburi[1]?

Jibu: Hakuna kipingamizi akiomba du´aa mmoja na wakaitikia “Aamiyn” wasikilizaji. Hapana vibaya ikiwa hilo halikupangwa. Imetokea wamesikia baadhi wakiomba du´aa na wengine wakaitikia “Aamiyn”. Hakuitwi kuwa ni du´aa ya pamoja kwa sababu ni kitu ambacho hakikupangwa.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/340).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 89
  • Imechapishwa: 15/01/2022