122. Wapi anapoelekea mtu anapomwombea du´aa maiti makaburini?

Swali 122: Je, kukatazwe kulielekea kaburi wakati wa kumwombea du´aa maiti[1]?

Jibu: Kusikatazwe. Bali maiti aombewe du´aa. Ni mamoja mtu ameelekea Qiblah au amelielekea kaburi. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisimama karibi na kaburi baada kuzika na akasema:

“Mwombeeni msamaha ndugu yenu na mtakieni uimara; kwani hakika hivi sasa anahojiwa.”[2]

Hakusema watu waelekee Qiblah. Kwa hiyo yote yanafaa. Ni mamoja mtu ataelekea Qiblah au Ka´bah. Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walimwombea du´aa maiti ilihali wamekusanyika pambizoni na kaburi.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/338).

[2] Abu Daawuud (3221).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 88-89
  • Imechapishwa: 15/01/2022