Mwenye kufikiria kwa kina basi ataona kuwa dunia hii ni safari. Atamwandaa mnyama wake kwa ajili ya safari. Anajua kuwa safari yake inaanza kutoka kwenye mgongo wa baba kwenda kwenye tumbo la mama, kisha kwenda duniani, halafu kwenda kaburini, kisha kwenda kufufuliwa na hatimaye katika maisha ya milele. Nyumba ya milele ni ile iliyosalimika na mabaya aina yote. Ni nyumba ya milele. Adui ndiye katufanya kuja katika dunia hii. Hetu tufanye bidii kujikwamua na kuanza safari yetu ya kurudi katika nyumba yetu ya kwanza.

Ni lazima wakati wa safari kuwa na masurufu. Hakuna masurufu mengine yatayoweza kukufikisha Aakhirah isipokuwa kumcha Allaah. Ni lazima mtu ataabike na asubiri juu ya uchungu wa kumcha Allaah ili wakati wa safari asije kusema “Nirudisheni!” Aje kuambiwa: “Kamwe!” Kwa hiyo azinduke yule mghafilikaji kutokana na uzembe wake.

Wakati wa safari Allaah (Ta´ala) huwaonyesha alama waja Wake ili kuwashtua wasije wakapinda kutokamana na njia iliyonyooka. Yule ambaye mnyama wake utapinda kutokamana na njia iliyonyooka na akaona mambo ya kumtisha basi haraka sana arudi kwa Allaah na kuiacha njia hiyo iliyopinda. Anatakiwa atubie kwa ajili ya maasi yake na alie kwa kuwa na moyo msusuwavu. Pindi atapozinduka kutoka katika uzembe wake ataona kuwa maisha ya dunia hii ni nyumba ya udanganyifu iliyojengwa juu ya uchafu.

Baadhi ya Salaf wamesema:

“Tahadharini na maisha ya dunia hii. Hakika ni uchawi mkubwa kuliko Haaruut na Maaruut. Haruut na Maaruut walikuwa wakitenganisha baina ya mume na mke. Ama dunia hii inamtenganisha mja na Mola wake.”

Himdi zote anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu. Swalah na salaam zimwendee bwana wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah wake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 247-249
  • Imechapishwa: 04/01/2017