122. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa pili wa al-An´aam

al-´Ayyaashiy amesema:

“Abu Hamzah ash-Shimaaliy amepokea kutoka kwa Abu Ja´far aliyesema kuhusiana na maneno ya Allaah (Ta´ala):

فَلَمَّا نَسُوا مَا ذُكِّرُوا بِهِ فَتَحْنَا عَلَيْهِمْ أَبْوَابَ كُلِّ شَيْءٍ حَتَّىٰ إِذَا فَرِحُوا بِمَا أُوتُوا أَخَذْنَاهُم بَغْتَةً فَإِذَا هُم مُّبْلِسُونَ

“Waliposahau yale waliyokumbushwa nayo, Tuliwafungulia milango ya [anasa za] kila kitu, mpaka walipofurahia kwa yale waliyopewa; tamahaki Tukawachukua [kwa kawaadhibu], basi mara wao wakawa wenye kukata tamaa.”[1]

 “Wakati walipoacha uongozi wa ´Aliy ambao waliamrishwa kushikamana nao, ndipo tukawachukua kwa kuwaadhibu, basi mara wao wakawa wenye kukata tamaa.  Imeteremshwa juu ya kizazi cha al-´Abbaas.”

Mansuur bin Yuunus amehadithia kutoka kwa mtu aliyesimulia ya kwamba Abu ´Abdillaah amesema: “Amewaadhibu Banuu Umayyah ghafla na Banuul-´Abbaas waziwazi.”[2]

Katika Aayah hii Allaah anamweleza Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) jinsi nyumati zilizotangulia zilivyoangamia. Allaah aliwatumia Mitume Wake ili wamuamini Yeye, wamuabudu, wamche na wamfuate Mtume Wake na Shari´ah Yake, lakini wakawakadhibisha na wakabaki ni wenye majivuno na kiburi. Ndipo Allaah akateremsha adhabu Yake kwa Ummah baada ya Ummah na akasema:

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا إِلَىٰ أُمَمٍ مِّن قَبْلِكَ فَأَخَذْنَاهُم بِالْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ لَعَلَّهُمْ يَتَضَرَّعُونَ فَلَوْلَا إِذْ جَاءَهُم بَأْسُنَا تَضَرَّعُوا وَلَـٰكِن قَسَتْ قُلُوبُهُمْ وَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ فَلَمَّا نَسُوا مَا ذُكِّرُوا بِهِ فَتَحْنَا عَلَيْهِمْ أَبْوَابَ كُلِّ شَيْءٍ حَتَّىٰ إِذَا فَرِحُوا بِمَا أُوتُوا أَخَذْنَاهُم بَغْتَةً فَإِذَا هُم مُّبْلِسُونَ فَقُطِعَ دَابِرُ الْقَوْمِ الَّذِينَ ظَلَمُوا ۚ وَالْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

“Hakika Tuliwapeleka Mitume kwa nyumati kabla yako, Tukawatia katika dhiki za ufukara na madhara ya magonjwa na misiba ili [wajifunze] kunyenyekea. Basi kwa nini ilipowafikia adhabu Yetu wasinyenyekee? Lakini nyoyo zao zilikuwa ngumu na shaytwaan akawapambia yale waliyokuwa wakitenda. Waliposahau yale waliyokumbushwa nayo, Tuliwafungulia milango ya [anasa za] kila kitu, mpaka walipofurahia kwa yale waliyopewa; tamahaki Tukawachukua [kwa kawaadhibu], basi mara wao wakawa wenye kukata tamaa. Basi ikakatwa mizizi ya watu waliodhulumu. – Himdi zote anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu.”[3]

 Maongezi yanahusiana na nyumati zilizowakadhibisha Mitume wao na wakayakufuru yale waliyokuja nayo. Kama mfano wa watu wa Nuuh, watu wa Huud, watu wa Swaalih, watu wa Ibraahiym, watu wa Luutw na watu wa Shu´ayb. Watu wa Fir´awn walimkadhibisha Muusa na wengineo.

Halafu anakuja huyu Baatwiniy na kuzipotosha na kuzipindisha Aayah hizi kutoka katika maana zake na malengo yake ambayo amekusudia Allaah na wakayafahamu waislamu na kwenda katika njama za Raafidhwah. Wanazusha mivutano ya kisiasa iliotokea kati ya kizazi cha Faatwimah na Maswahabah, Banuu Umayyah, Banuul-´Abbaas na Ummah mzima. Si kizazi cha Faatwimah wala Ummah mzima hautaki jambo hilo. Wameipotosha Qur-aan na wameifanya historia ya Kiislamu kuonekana vibaya kwa ajili ya jambo hilo.

[1] 06:44

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/360).

[3] 06:42-45

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 179-180
  • Imechapishwa: 12/06/2018