121. Takbiyr wakati wa kurusha vijiwe katika nguzo

  Download

239-

“Atasema:

أَللّهُ أَكْبَرُ

“Allaah ni mkubwa.”

kila ambapo atarusha vijiwe kwenye nguzo tatu. Kisha atasogea mbele ambapo atasimama na akiomba du´aa hali ya kuelekea Qiblah, akinyanyua mikono yake baada ya kiguzo cha kwanza na cha pili. Ama kuhusu kiguzo cha tatu,  atarusha na kusema:

أَللّهُ أَكْبَرُ

“Allaah ni mkubwa.”

wakati wa kila kijiwe na kisha aondoke na asisimame mahala hapo.”[1]

[1] al-Bukhaariy pamoja na al-Fath (03/583-584) na (03/584). Tazama tamko lake huko. Pia al-Bukhaariy pamoja na al-Fath (03/581) na Muslim ameipokea pia.

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 09/05/2020