121. Kunyanyua mikono wakati wa kumwombea du´aa maiti

Swali 121: Je, du´aa inayoombwa karibu na kaburi inakuwa kwa kunyanyua mikono[1]?

Jibu: Hapana vibaya endapo atanyanyua mikono. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ya kwamba:

“Aliyatembelea makaburi ambapo akanyanyua mikono na akawaombea du´aa watu wake.”[2]

Ameipokea Muslim.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/337).

[2] Muslim (974).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 88
  • Imechapishwa: 15/01/2022