121. Alama ya mwenye furaha na mla khasara

Imethibiti katika “as-Swahiyh” ya Muslim kupitia kwa al-Mustawrid bin Shaddaad an-Fahriy ya kwamba alimsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Dunia hii ukiilinganisha na Aakhirah ni kama mmoja wenu kuchukua kidole chake akakiweka ndani ya bahari. Atazame kitatoka na nini.”

´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mwenye kuipa nyongo dunia misiba huwa ni miepesi kwake. Mwenye kuona kifo kiko karibu basi hukimbilia kufanya matendo ya kheri.”

al-Hasan al-Baswriy amesema:

“Ninaapa kwa yule Ambaye nafsi yangu iko mkononi Mwake nilikutana na watu waliokuwa wakiichukulia sahali dunia hii kuliko ardhi ambao nyinyi mnatembea juu yake.”

Alama ya kula khasara ni kuwa na moyo mgumu, macho makavu, mipango mikubwa ya huko mbele na kuyapupia maisha ya dunia hii. al-Fudhwayl bin ´Iyaadhw amesema:

“Alama ya furaha ni kuwa na yakini moyoni, unyenyekevu katika dunia, kuyapa nyonyo maisha haya ya dunia, kuwa na haya na elimu.”

al-Fudhwayl amesema tena:

“Lau ningeipata dunia yote na vizuri vyake pasi na kufanyiwa hesabu kwayo huko Aakhirah, basi ningeliiepuka kama mnavyoepuka nyamafu asiziguse nguo zenu.”

Abu Haashim amesema:

“Allaah ameumba ugonjwa na dawa. Ugonjwa ni dunia hii na dawa ni kule mtu kuiacha.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 244-246
  • Imechapishwa: 03/01/2017