120. Maisha ni yenye furaha ndogo na masononeko mengi

Tambua kwamba uovu wa maisha ya dunia hii ni kama ndoto mbaya au kivuli chenye kuondoka. Hata kama yatamfanya mtu kucheka kidogo basi yatamfanya vilevile kulia sana. Hata kama yatamfanya mtu kufurahi baadhi ya siku basi yatamfanya vilevile kuhuzunika miezi na miaka. Kama yanatoa sana inazuia sana vilevile. Furaha yote anayopata mja ndani yake inafunikwa na masononeko. Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Kila furaha ina huzuni. Hakuna nyumba iliyojaa furaha isipokuwa hujaa huzuni.”

Ibn Siyriyn amesema:

“Hakuna mwenye kucheka isipokuwa hulia baada yake.”

Binti wa an-Nu´maan amesema:

“Siku moja niliona kuwa sisi ndio watu watukufu na wenye ufalme mkubwa. Jua halikuwahi kuzama kabla ya sisi kujiona kuwa ni watu watwevu zaidi. Ni haki ya Allaah (´Azza wa Jall) kutoijaza nyumba wino isipokuwa Huijaza pia mazingatio.”

Imepokelewa kuwa ´Iysaa (´alayhis-Salaam) amesema:

“Ole wake yule anayeikimbilia dunia hii! Vipi atakufa na kuiacha? Anajiaminisha nayo na inamughuri. Anaiamini na inamkosesha nusura. Ole wao wale wenye kudanganyika! Wanasogelewa na kile wanachokichukia. Wamefarikiana na kile wanachokipenda. Wamejiwa na kile walichoahidiwa. Ole wake yule ambaye hamu yake kubwa ni hii dunia na ambaye matendo yake ni madhambi! Ni vipi atafedhekea kesho kwa ajili ya madhambi yake?”

Ibn Abid-Dunyaa amepokea kupitia kwa Wahb bin Munabbih kwamba ´Iysaa (´alayhis-Salaam) amesema:

“Nawaelezeni ukweli. Kama ambavyo mgonjwa anakitazama chakula kizuri lakini hahisi hamu nacho kutokana na ukubwa wa maumivu vivyo hivyo yule anayeipupia dunia hahisi ladha ya ´ibaadah. Hahisi utamu kutokana na yale mapenzi yake makubwa ya dunia hii. Ikiwa mnyamwa hapandwi na kunyenyekezwa anakuwa ni mgumu kumwelekeza na maumbile yale yanabadilika. Kadhalika mioyo. Ikiwa hailainishwi kwa kuyakumbuka mauti na kumuabudu Allaah daima inakuwa migumu na susuwavu.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 244-245
  • Imechapishwa: 01/01/2017