12. Wenye janaba wanatakiwa kutawadha kabla ya kulala

10- Mwenye janaba kutawadha kabla ya kulala

Wenye janaba wasilale isipokuwa baada ya kutawadha. Kumekuja Hadiyth juu ya hilo:

1- ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia akisema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa anataka kula au kulala ilihali yuko na janaba, basi anaiosha tupu yake na kutawadha wudhuu´ wa swalah.”[1]

2- Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia:

“´Umar aliuliza: “Ee Mtume wa Allaah! Je, mmoja wetu alale ilihali yuko na janaba?” Akamjibu: “Ndio, akitawadha.”

Katika upokezi mwingine imekuja:

“Tawadha kisha osha dhakari yako halafu lala.”

Katika upokezi mwingine imekuja:

“Ndio, atawadhe kisha asilale mpaka kwanza aoge pale atapotaka.”

Katika upokezi mwingine imekuja:

“Ndio, na atawadhe akitaka.”

3- ´Ammaar bin Yaasir (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watu watatu Malaika hawawakaribii; maiti ya kafiri, mwenye kujitia manukato ya wanawake na mwenye janaba isipokuwa akitawadha.”[2]

[1] Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim na Abu ´Awaanah katika “as-Swahiyh” zao. Nimeipokea katika kitabu changu “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (218).

[2] Hadiyth ni nzuri. Ameipokea Abu Daawuud katika “Sunan” yake (02/192-193) kupitia njia ya Ahmad, at-Twahaawiy, al-Bayhaqiy katika moja wapo na ni Swahiyh kwa mujibu wa at-Tirmidhiy na wengineo. Kuna mtazamo fulani ambao nimeubainisha katika kitabu changu “Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” kwa nambari. 29. Lakini matini ya njia ya kwanza – ambayo ni hii – ina shawahidi ambazo zimepokelewa na al-Haythamiy katika “al-Jaamiy´” (05/156). Kwa ajili hii ndio maana nimeonelea kuwa ni nzuri. Njia nyingine imepokelewa na at-Twabaraaniy katika “al-Kabiyr” (02/143/03) kupitia Hadiyth ya Ibn ´Abbaas.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 114-115
  • Imechapishwa: 08/03/2018