12. Wanatafuta makosa ya watawala na kuwavugumizia tuhuma wanachuoni

12- Wanatafuta makosa ya watawala katika miji ya Kiislamu kwa jumla na khaswa watawala wa nchi hii. Wanatupa tuhuma mbaya dhidi ya wanachuoni wa Salafiyyah katika nchi hiyo na kuwatuhumu kwamba ni vibaraka wanaofanya kazi chini ya shinikizo na kwamba hawafahamu mambo ya kisasa. Wanadai kuwa ghera yao juu ya Uislamu imekufa na kwamba sio marejeleo ya kielimu katika nchi hii[1].

[1] Imaam Swaalih al-Fawzaan amesema:

“Kijitabu hichi kilichoko mbele yetu kimeandikwa na ndugu yetu Shaykh Zayd bin Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy. Kinatahadharisha mifumo hii, kinabainisha athari zake mbaya na kinahimiza kushikamana barabara na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Allaah amjaze kheri na anufaishe kwa nasaha na maelekezo yake.” (Asbaab Istiqaamat-ish-Shabaab wa Bawaa´ith Inhiraafihim, uk. 7)

 

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Asbaab Istiqaamat-ish-Shabaab wa Bawaa´ith Inhiraafihim, uk. 20
  • Imechapishwa: 25/03/2017