Swali 12: Je, makundi haya yanaingia ndani ya yale mapote sabini na mbili yaliyoangamia?

Jibu: Ndio, kila mwenye kujinasibisha na Uislamu na akaenda kinyume na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah katika ulinganizi, ´Aqiydah au kitu kingine katika misingi ya imani basi anaingia ndani ya yale mapote sabini na mbili. Wanajumuishwa na matishio. Wanasimangwa na kuadhibiwa kwa kiwango cha uhalifu wao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 35
  • Imechapishwa: 08/04/2017