12. Wanaingia katika mapote sabini na mbili


Swali 12: Je, makundi haya yanaingia katika mapote sabini na mbili yaliyoangamia?

Jibu: Ndio, kila mwenye kujinasibisha na Uislamu na anaenda kinyume na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah katika Da´wah, ´Aqiydah au kitu kingine katika misingi ya imani anaingia katika mapote sabini na mbili. Wanaguswa na matishio. Wanalaumiwa na kuadhibiwa kwa kiasi cha uhalifu wao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Adjwibah al-Mufiydah ´an As'ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 35
  • Imechapishwa: 08/04/2017