12. Wafanyakazi wa mahospitali mwanaume kukaa faragha na mwanamke

Swali 12: Mimi ni muuguzi ambaye ninafanya kazi ya kuwauguza wanaume. Kwenye kitengo changu kuna muuguzi mwanamke ambaye ninafanya naye kazi katika wakati baada ya masaa ya kazi rasmi na kazi inaendelea wakati mwingine mpaka alfajiri. Wakati mwingine kunatokea kikamilifu kukaa naye faragha. Tunachelea juu ya nafsi zetu fitina na hatuwezi kubadilisha hali hii. Je, tuache kazi kwa ajili ya kumcha Allaah ilihali hatuna kazi nyingine kwa ajili ya kuchuma riziki?

Jibu: Haijuzu kwa wale wasimamizi wa mahospitali kuweka muuguzi mwenye kazi ya kudumu na muuguzi mwanamke wakakesha usiku wakiwa wao wenyewe kwa ajili ya kuchunga. Hili ni kosa na maovu makubwa. Kitendo hichi maana yake ni kuita katika machafu. Mwanaume akiachwa sehemu moja faragha na mwanamke, basi hakuaminika juu yao shaytwaan akawapambia kufanya machafu na njia zake. Kwa ajili hiyo imesihi ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanaume hakai faragha na mwanamke isipokuwa watatu wao anakuwa ni shaytwaan.”

Kitendo hichi hakifai. Ni lazima kwako kukiacha kwa sababu ni haramu na kinapelekea katika yale aliyoharamisha Allaah (´Azza wa Jall). Allaah atakupa bora kuliko hiyo ikiwa utaiacha kwa ajili ya Allaah. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ

“Na yeyote anayemcha Allaah, basi atamjaalia njia ya kutoka.” (65:02-03)

وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مِنْ أَمْرِهِ يُسْرًا

“Na yeyote anayemcha Allaah, basi atamjaalia wepesi katika jambo lake.” (65:05)

Vivyo hivyo kwa muuguzi huyo mwanamke ni lazima kwake kutahadhari na hilo na ajiuzulu kazi ikiwa hakuna njia nyingine. Kwa sababu kila mmoja kati yenu ataulizwa juu ya yale aliyomuwajibishia Allaah juu yake na yale aliyomuharamishia juu yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Mariydhw, uk. 33-35
  • Imechapishwa: 06/07/2019