12. Ulipuaji ´Ulayyaa ni mfano wa ugaidi

11- Kwa hiyo ulipuaji mbaya uliofanywa na genge shambulizi na haribifu siku ya jumatatu tarehe 20 Jumaadaa al-Aakhir mwaka 1416 sehemu ya mji wa ´Ulayyaa ar-Riyaadh ni mfano wa ugaidi. Tendo hilo lilishtua nchi nzima na mambo yalikuwa mabaya zaidi wakati ilipodhihiri kuwa wahalifu walikuwa ni wasaudi waliokuwa wameathiriwa na mikanda iliokuwa imezichochea hisia zao na kuvijaza vifua vyao chuki dhidi ya watawala wa waislamu na wanachuoni wanaofuata mfumo wa kiutume. Matokeo yake wakapanga jinai la kidhambi na ovu ambalo hakuna yeyote aliyekuwa akilitarajia.

Nafsi zisizokuwa na hatia ambazo zilikuwa na haki ya usalama zikafa katika nchi ya Kiislamu. Mali tukufu ikatokomea. Lakini hata hivyo wahalifu hawaelewi. Wakakamatwa na kutekelezewa Shari´ah tukufu. Ardhi ikatwahirika kutokamana na ufisadi wao na wakaenda kwa Mola wao wakiwa na madhambi yao juu ya migongo yao. Tunamuomba Allaah atukinge na mwisho mbaya.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Irhaab, uk. 19-20
  • Imechapishwa: 03/04/2017