12. Ugeni wa Uislamu na ubora wa wageni

Allaah (Ta´ala) amesema:

فَلَوْلَا كَانَ مِنَ الْقُرُونِ مِن قَبْلِكُمْ أُولُو بَقِيَّةٍ يَنْهَوْنَ عَنِ الْفَسَادِ فِي الْأَرْضِ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّنْ أَنجَيْنَا مِنْهُمْ ۗ وَاتَّبَعَ الَّذِينَ ظَلَمُوا مَا أُتْرِفُوا فِيهِ وَكَانُوا مُجْرِمِينَ

“Basi kwanini hawakuweko katika karne za kabla yenu, watu weledi wanakataza ufisadi katika ardhi isipokuwa wachache kati ya Tuliowaokoa miongoni mwao! Na wale waliodhulumu wakafuata [anasa] walizostareheshwa nazo na wakawa wahalifu.” (11:116)

Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Uislamu ulianza ni kitu kigeni na utarudi kuwa kitu kigeni kama ulivyoanza. Hivyo Twubaa kwa wale wageni!”[1]

Ameipokea Muslim.

Ahmad amepokea kupitia kwa Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa:

“Ni kina nani wageni?” Akajibu: “Ni watu wachache katika makabila.”[2]

Katika upokezi mwingine imekuja:

“Wageni ni wale wanaotengeneza pale wanapoharibika watu.”[3]

Ahmad amepokea kupitia kwa Sa´d bin Abiy Waqqaas kwa muundo:

“Twubaa kwa wageni siku ambayo watu wameharibika!”

at-Tirmidhiy amepokea kupitia kwa Kathiyr bin ´Abdillaah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake kwa muundo:

“Twubaa kwa wageni wenye kutengeneza yale waliyoharibu watu katika Sunnah zangu!”[4]

Abu Umayyah amesema:

“Nilimuuliza Abu Tha´labah al-Khushaniy (Radhiya Allaahu ´anh) juu ya Aayah:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَيْكُمْ أَنفُسَكُمْ ۖ لَا يَضُرُّكُم مَّن ضَلَّ إِذَا اهْتَدَيْتُمْ

“Enyi mlioamini! Ni juu yenu [majukumu ya] nafsi zenu. Hawakudhuruni waliopotoka, ikiwa mmeongoka.” (05:105)

Akajibu: “Ninaapa kwa Allaah ya kwamba mimi mwenyewe nilimuuliza nayo mtu mjuzi; nilimuuliza Mtume wa Allaah na akasema: “Mtaamrishana mema na kukatazana maovu. Pindi mnapoona choyo inayotiiwa, matamanio yanayofuatwa, dunia inayopewa kipaumbele na jinsi kila mmoja anavyopendekeza maoni yake, basi hapo shikamana na nafsi yako na uachane watu wajinga. Mbele yenu kunakuja masiku ambayo mwenye subira ni kama mfano wa aliyeshika kaa [la moto] na mtendaji mwenye kutenda kama nyinyi analipwa ujira wa wanaume khamsini.” Tukasema: “Katika sisi au katika wao?” Akasema: “Katika nyinyi.”[5]

Ameipokea Abu Daawuud na at-Tirmidhiy.

Ibn Wadhdhwaah amepokea maana kama hiyo kutoka kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kwa muundo:

“Baada yenu kunakuja masiku ambayo yule aliyeshikamana na yale mnayofanya nyinyi hii leo analipwa ujira wa wanaume khamsini katika nyinyi.”

Kisha akasema: “Muhammad bin Sa´iyd ametueleza: Asad ametueleza: Sufyaan bin ´Uyaynah ametukhabarisha, kutoka kwa Aslam al-Baswriy, kutoka kwa Sa´iyd, nduguye al-Hasan, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Nilisema kumwambia Sufyaan: ”Haya yanatoka kwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?” Akasema: “Ndio.” Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hii leo mko katika ushahidi wa wazi kutoka kwa Mola Wenu, mnaamrisha mema, mnakataza maovu na mnapigana Jihaad katika njia ya Allaah na hamjasibiwa na vilevi viwili ambacho ni kilevi cha ujinga na kilevi cha kupenda maisha. Hata hivyo mtakuja kubadilika muache kuamrisha mema, kukataza maovu, kupigana Jihaad kwa ajili ya Allaah na mtasibiwa na vilevi viwili. Siku hiyo yule mwenye kushikamana barabara na Kitabu na Sunnah analipwa ujira khamsini.” Wakasema: “Katika sisi?” Akasema: “Hapana. Katika nyinyi.”[6]

Amepokea kwa mlolongo wa wapokezi kupitia kwa al-Mu´aafiriy ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Twubaa kwa wageni wenye kushikamana na Kitabu pindi kinapoachwa na wanaitendea kazi Sunnah pindi inapozimwa!”[7]

[1] Muslim (145).

[2] Ahmad (1/398).

[3] Zawaa’id-ul-Musnad (4/73).

[4] at-Tirmidhiy (2630) ambaye amesema: ”Hadiyth ni Hasan na Swahiyh.”

[5] Abu Daawuud (4341), at-Tirmidhiy (3058) na Ibn Maajah (4014).

[6] al-Bid´ah, uk. 133.

[7] al-Bid´ah, uk. 122.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-ul-Islaam, uk. 39-41
  • Imechapishwa: 23/10/2016