Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Sharti ya tisa ni nia na mahala pale ni moyoni. Kuitamka ni Bid´ah. Dalili ni Hadiyth:

“Matendo huzingatiwa kwa nia. Kila mmoja atalipwa kutokana na kile alichonuia.”[1]

MAELEZO

´Ibaadah zote ni lazima kwa mtu azitilie nia; kama mfano wa swalah, swawm na nyenginezo. ´Ibaadah zote ni lazima kwa mtu azitilie nia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Matendo huzingatiwa kwa nia. Kila mmoja atalipwa kutokana na kile alichonuia.”

Nia mahala pake ni moyoni. Mahala pa nia katika swalah, swawm na ´ibaadah nyenginezo ni kwenye moyo. Isipokuwa katika hajj. Katika hajj anatakiwa kuisema kwa sauti ule mtindo wa ´ibaadah aliochagua. Hivo ndivo alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama ´ibaadah zengine zote nia iko moyoni.

Kuitamka ni Bid´ah. Kutamka nia kwamba mtu anataka kuswali, anataka kufunga au anataka kutoa swadaqah ni Bid´ah. Isipokuwa tu katika hajj ndio Shari´ah imekuja ikionyesha kudhihirisha Ihraam ya mtu na kusema:

لبيك عمرة

”Nakuitikia ´Umrah.”

لبيك حجا

”Nakuitikia Hajj.”

لبيك عمرة و حجا

”Nakuitikia ´Umrah na Hajj.”

Adhihirishe nia yake iliyomo moyoni. Hii ni Sunnah na kama tulivosema ni jambo maalum katika hajj na ´umrah.

[1] al-Bukhaariy (1) na Muslim (1907).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 83-84
  • Imechapishwa: 30/06/2018