12. Njia ya tano: uwajibu wa kuzitambua njia za kuifikia elimu sahihi

Katika njia za kuipata elimu ni kuzitambua zile njia za kuifikia. Hakika jambo hili ni miongoni mwa mambo muhimu na yenye manufaa kwa mwanafunzi.

Baadhi ya wanafunzi wanapita katika njia zao za kutafuta elimu kama mfano wa mwenye kwenda kuogelea kwenye bahari bila ya kujua namna ya kuogelea. Matokeo yake anakuwa si mwenye kujua wala kupata elimu yoyote. Sababu ya hilo hakujua njia ya kupita.

Ndugu wapenzi! Ni lazima tujue njia sahihi yenye kuchukuliwa kutoka kwa as-Salaf as-Swaalih katika kuipata elimu ya Kishari´ah.

Miongoni mwa mambo muhimu kabisa ni kuanza na mambo madogo kabla ya makubwa. as-Salaf as-Swaalih walikuwa wakimkataza mwanafunzi kuanza na mambo makubwa kabla ya madogo. Unapotaka kuanza kusoma fani fulani, panga vitabu vyake ambapo vitabu vinakuwa vimepangika ifuatavyo: vitabu vifupi, vitabu vya kati na kati na vitabu vikubwa. Katika fani hii [unayotaka kusoma] anza kwa vitabu vifupi na uchague kile kitabu ambacho wanachuoni wamekitumikia sana ambacho utaweza kwenda nacho mpaka njia ya mwisho. Usome kitabu hichi kifupi, uyaelewe yaliyomo ndani yake, uelewe maana yake na hatimae uitambue elimu hii. Baada ya hapo uende katika kitabu kilicho kati na kati na ufanye hali kadhalika. Kisha baada ya hapo uende katika kitabu kikubwa. Yote haya unayafanya kwa kusoma chini ya mwalimu mwenye uelewe na ambaye ni msomi kwa yale unayoyasoma na wakati huo huo ni mjuzi juu ya yale anayoyasema. Hakika katika kufanya hivo kuna kheri kubwa. Ambaye atapita njia hii basi atafikia kheri na kuwa imara. Ambaye hatopita mapito haya anaweza kuwa mwanautamaduni, lakini hata hivyo hatokuwa mwanachuoni na hatofikia elimu imara itayobaki kwenye nafsi yake.

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Ilm wa Wasaaailuh wa Thimaaruh
  • Imechapishwa: 22/10/2016