Mwandishi amesema:

“Sisi sote tunamwamini mungu mmoja.”

Haya yanawahusu waislamu ambao wanamwamini mwabudiwa Mmoja, wanamwabudu Yeye Mmoja na wananyenyekea juu ya Shari´ah Yake. Naye si mwengine ni Allaah (´Azza wa Jall) ambaye ndiye muumba wa mbingu na ardhi, muumba wa kila kitu na Mola wa kila kitu ambaye amesema:

وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ

“Mungu wenu ni Mungu mmoja pekee; hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Yeye, Mwingi wa huruma, Mwenye kurehemu.”[1]

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ يَطْلُبُهُ حَثِيثًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ َ

“Hakika Mola wenu ni Allaah ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ´Arshi. Anafunika usiku kwa mchana, unaufuatia upesi upesi na [ameumba] jua na mwezi.”[2]

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ

”Allaah, hapana mungu wa haki isipokuwa Yeye, Aliyehai daima, Mwenye kusimamia kila kitu. Haumchukui usingizi wala kulala. Ni Vyake pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Nani huyu ambaye anaombea mbele Yake bila ya idhini Yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawakizunguki chochote katika elimu Yake isipokuwa kwa akitakacho. Kursiy Yake imeenea mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye yujuu kabisa, Ametukuka.”[3]

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ اللَّـهُ الصَّمَدُ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ

“Sema: ”Allaah ni Mmoja pekee, Mwenye kutegemewa kwa haja zote, hakuzaa na wala hakuzaliwa na wala haiwi awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye.”[4]

Mayahudi na manaswara wanamwabudu Allaah pamoja na waungu wengine. Hawamwabudu mungu Mmoja. Amesema (Ta´ala):

لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ ۘ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۚ وَإِن لَّمْ يَنتَهُوا عَمَّا يَقُولُونَ لَيَمَسَّنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

“Kwa hakika wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni watatu wa utatu.” Ilihali hakuna mungu wa haki isipokuwa Mmoja Pekee. Na wasipoacha yale wanayoyasema, bila ya shaka itawagusa wale waliokufuru miongoni mwao adhabu iumizayo.”[5]

وَقَالَتِ الْيَهُودُ عُزَيْرٌ ابْنُ اللَّـهِ وَقَالَتِ النَّصَارَى الْمَسِيحُ ابْنُ اللَّـهِ ۖ ذَٰلِكَ قَوْلُهُم بِأَفْوَاهِهِمْ ۖ يُضَاهِئُونَ قَوْلَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَبْلُ ۚ قَاتَلَهُمُ اللَّـهُ ۚ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ وَالْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا إِلَـٰهًا وَاحِدًا ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ سُبْحَانَهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ

”Mayahudi wanasema ”‘Uzayr ni mwana wa Allaah” na manaswara wanasema ”al-Masiyh ni mwana wa Allaah” Hiyo ni kauli yao kwa midomo yao. Wanayaiga maneno ya wale waliokufuru kabla. Allaah awaangamize! Ni vipi wanageuzwa? Wamewafanya marabi wao na watawa wao kuwa ni waungu badala ya Allaah na al-Masiyh, mwana wa Maryam, ilihali hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Mungu Mmoja pekee. Hapana mungu wa haki isipokuwa Yeye. Utakasifu ni Wake kutokamana na yale yote wanayomshirikisha nayo.”[6]

 Amebainisha (Subhaanah) kupitia Aayah hizi kwamba mayahudi na manaswara wamewaabudu waungu wengi katika marabi na watawa. Mayahudi wamemwabudu al-´Uzayr na wakadai kuwa ni mwana wa Allaah. Manaswara wamemwabudu al-Masiyh mwana wa Maryam na wakadai kuwa ni mwana wa Allaah na kwamba wote hawakuamrishwa jengine isipokuwa kumwabudu mungu Mmoja. Naye si mwengine ni Allaah (Subhaanah) ambaye ndiye muumba wa kila kitu na mlezi wa wote – ametakasika kutokamana na yale wanayomshirikisha.

[1] 02:163

[2] 07:54

[3] 02:255

[4] 112:01-04

[5] 05:73

[6] 09:30-31

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/articles/78/الاسلام-هو-دين-الله-ليس-له-دين-سواه
  • Imechapishwa: 07/10/2021