12. Mke mwema daima anakuwa katika muonekano mzuri

6 – Ajionyeshe kwa mume wake kwa hali nzuri zaidi kwa njia ya kwamba pale anapomtazama basi anamfurahisha. Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu anh) ameeleza: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa: “Ni mwanamke yupi bora?” Akasema:

“Ni yule ambaye anamfurahisha [mume] anapomtazama, anamtii anapomwamrisha, hapingani naye katika nafsi yake na mali yake kwa yanayomchukiza.”[1]

[1] an-Nasaa´iy (06/67), al-Haakim (02/61), Ahmad (02/251, 432, 437). al-Haakim amesema:

“Swahiyh juu ya sharti za Muslim.” ambapo adh-Dhahabiy akaafikiana naye. al-´Iraaqiy amesahihisha cheni ya wapokezi wake katika “Takhriyj-ul-Ihyaa´” (02/39). Ni nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “as-Swahiyhah” (04/453).

  • Mhusika: Shaykh Muhammad Shuwmaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 29
  • Imechapishwa: 27/09/2022