12. Mke mwema anatakiwa kubaki nyumbani


Katika sifa za mke mwema ni kwamba anatakiwa kutulizana nyumbani na hawi ni mwenye kutokatoka na kuingia nyumbani kila wakati. Anapotoka basi hatoki isipokuwa kwa haja. Anapotoka hawi ni mwenye kujipodoa na kuonyesha mapambo na uso ukiwa wazi. Vilevile anatakiwa kuteremsha chini macho yake na kuhifadhi tupu yake. Tumekwishapitia baadhi ya maandiko kuhusu hilo. Moja katika dalili ni yale ambayo at-Twabaraaniy amepokea katika “al-Awsaatw”[1] kupitia Saalim bin ´Abdillaah bin ´Umar kutoka kwa baba yake ambaye ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanamke ni ´Awrah. Wakati anapotoka nje basi Shetani humpamba. Anakuwa yukaribu zaidi na Allaah pindi anapokuwa ndani kabisa ya nyumba yake.”

[1] 2890 och 8096. Imaam al-Albaaniy amesema kuwa ni Swahiyh katika ”as-Swahiyhah” (2688).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 41-42
  • Imechapishwa: 20/08/2018