Allaah (Ta´ala) amesema:

فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ

“Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi mpya na afunge.”[1]

Hii ni amri kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall). Amri ni wajibu. Ina maana kwamba yule ambaye yuko katika mji wake pindi mwezi uandamapo basi ni wajibu kwake kufunga. Hapa ni pale ambapo atakuwa ni muweza, kishabaleghe na ni mwenye akili. Ikikosekana moja katika masharti haya basi sio wajibu kwake kufunga.

Swawm maana yake ni mtu kujiepusha na vile vinavyofunguza kuanzia pale ambapo alfajiri ya pili inapoingia mpaka pale jua linapozama kwa kunuia kufunga. Kwa msemo mwingine swawm inatakiwa kutekelezwa na mtu aliye na akili. Haiwezekani kufunga wala kufanya ´ibaadah kwa aliyekosa akili. Hapana shaka ya kwamba swawm ni faradhi na nguzo moja wapo ya Uislamu. Haya ni kwa maafikiano ya waislamu.

[1] 02:185

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tafsiyr Aayaat-is-Swiyaam, uk. 23-24
  • Imechapishwa: 02/06/2017