1 – Miaka michache ambayo mwanamke hupata hedhi mara nyingi huwa ni tisa mpaka miaka khamsini. Amesema (Ta´ala):

وَاللَّائِي يَئِسْنَ مِنَ الْمَحِيضِ مِن نِّسَائِكُمْ إِنِ ارْتَبْتُمْ فَعِدَّتُهُنَّ ثَلَاثَةُ أَشْهُرٍ وَاللَّائِي لَمْ يَحِضْنَ

“Wale wanawake wanaokoma hedhi miongoni mwa wanawake wenu, mkiwa mna shaka, basi eda yao ni miezi mitatu, pamoja na wale wanawake wasiopata hedhi.”[1]

Wale waliokata tamaa ni wale waliofikisha miaka khamsini na wale ambao hawajapata hedhi ni wale wadogo walio chini ya miaka tisa.

[1] 65:04

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 27
  • Imechapishwa: 24/10/2019